Uchunguzi wa vinasaba umethibitisha kuwa Faru John alikufa. Sampuli zilizotumika katika vipimo ni mifupa, pembe, damu, ngozi na kinyesi.
Ni kwamujibu wa Ripoti aliyokabidhiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Tume aliyounda kuchunguza kifo cha Faru John kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele.
Hatua ya uchunguzi huo ilifuata baada ya Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa kuwataka maafisa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), kutoa ufafanuzi kuhusu kuhamishwa kwa faru maarufu kwa jina la John kutoka kwenye hifadhi hiyo.
Bw Majaliwa aliwataka viongozi wa NCAA kuwasilisha kwake nyaraka zote zilizotumika katika kumuhamisha faru huyo katika kipindi cha wiki moja.
Alisema ana taarifa kuwa faru huyo John alihamishwa kwa siri na kupelekwa Grumeti katika eneo Serengeti mnamo 17 Desemba, 2015.
"… mliahidiwa kupewa shilingi milioni 200 ambapo mkapewa shilingimilioni 100 kwa ahadi ya kumaliziwa shilingi milioni 100 nyingine baadaye," alisema Bw Majaliwa.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily News la Tanzania, Bw Majaliwa alisema kwa miezi mitatu sasa, hakuna taarifa zozote kumhusu faru huyo ambazo zimetolewa.
"Naomba niletewe nyaraka zote zilizotumika kumuomba na kumuondoa faru huyo na barua zilizotumika kujadili suala la faru John. Nasikia amekufa naomba pembe ziletwe ofisini na iwapo itathibitika aliondoka bila ya kufuata taratibu wahusika wote watachukuliwa hatua kali za kisheria,".
Bw Majaliwa pia alimsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa NCAA, Sezzary Simfukwe kutokana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha zinazomkabili.
Ambapo alihojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
"Haiwezekani mtumishi awe anachunguzwa na Takukuru halafu aendelee kuwa ofisini si atavuruga uchunguzi. Asimamishwe kazi kuanzia leo mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika na aikibainika kwamba hana hatia atarudi kazini," alisema.
Hifadhi ya Ngorongoro ndilo eneo pekee Tanzania ambapo faru wanapatikana kwa wingi porini, ndani ya kreta.
Inakadiriwa kwamba idadi ya faru katika hifadhi hiyo ni takriban 35.
0 Komentar untuk "HAYA NDIO MAJIBU KAMILI KUHUSU "FARU JOHN""