SERIKALI KUWAHAMISHA WALIMU 7,463 KUTOKA SHULE ZA SEKONDARI KWENDA MSINGI




Kero ya upungufu wa Walimu shule za Msingi imeanza kupatiwa ufumbuzi kufuatia Serikali kuja na mpango wa kuwahamisha walimu wa ziada katika masomo ya sanaa kwenye shule za sekondari wapatao 7,463 kwenda shule za msingi ili kupunguza upungufu na kuboresha elimu hiyo ya msingi.
Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Elimu, Bernard Makali mbele ya Kamati ya Kudumu Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati kamati hiyo ilipokuwa ikichambua taarifa za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Kamati ilikuwa inakagua taarifa hiyo kuhusu ufanisi katika Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi.
Makali alisema katika sekondari walimu wa sanaa (Arts) ni wengi kwa idadi hiyo ya zaidi ya 7,000 na kwamba hao wanaohamishwa wanachochea ubora wa elimu katika shule za msingi na marupurupu yao na mishahara itabaki kama

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Komentar untuk "SERIKALI KUWAHAMISHA WALIMU 7,463 KUTOKA SHULE ZA SEKONDARI KWENDA MSINGI"

Back To Top