ASKARI POLISI SABA WA WAUAWA KINYAMA NA MAJAMBAZI NA BUNDIKI ZAO KUPORWA






Jeshi la Polisi nchini limepata pigo  kufuata Askari wake saba waliokuwa katika doria kijiji cha Jaribu mpakani mwa wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani kuuawa kwa kupigwa risasi usiku wa Aprili 13,2017.

Kwa mujibu wa taarifa za awali zimebainsha kuwa polisi hao walikuwa kwenye gari wakirejea kituoni kutoka kwenye doria na walishambuliwa na watu waliotokea msituni.

Naye Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania IGP Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa taarifa zaidi zitatolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Pwani.

Imeelezwa kuwa majambazi hao waliwavamia ghafla polisi hao waliokuwa kwenye gari na kuwapiga risasi na kuwaua wote palepale eneo la tukio, kisha kutokomea kusikojulikana na kwamba silaha zote walizokuwa nazo (SMG) zilichukuliwa na watu hao.


Mkoa wa Pwani umekithiri matukio ya kiuhalifu pamoja na baadhi ya watu kuuawa na majambazi mara kwa mara, hivyo basi Jeshi la Polisi linapaswa kuongeza nguvu katika kulinda usalama wa raia na mali zao.

AHSANTE  KWA KUENDELEA KUSOMA HABARI KATIKA BLOG YETU 
ILI KUPATA HABARI KWA WEPESI ZAIDI LIKE PAGE YETU YA kiraminews
 
ILI KULIKE PAGE YETU bonyeza hapa


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Komentar untuk "ASKARI POLISI SABA WA WAUAWA KINYAMA NA MAJAMBAZI NA BUNDIKI ZAO KUPORWA "

Back To Top