HAYA NDIO MAGIZO ALIOTOA MWIGULU NCHEMBA KWA POLISI KUHUSU SAKATA LA KUTEKWA KWA ROMA




Msanii wa hip hop Roma Mkatolikia alikamatwa April 5 usiku ambapo taarifa zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kuwa alikamatwa studio za Tongwe Records  na watu wasiojulikana akiwa na wenzake na wakapelekwa  kusikojulikana.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ambaye ndio anahusika na usalama wa raia, ametumia ukurasa wake wa instagram na twitter kuonesha kuguswa na tukio la kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Moni.
Waziri Nchemba ameeleza kuwa amewaagiza polisi kufuatilia na kutoa taarifa kwa umma.

“Nimeshtushwa kwa kutokuonekana kwa Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa. Nimeshtuka zaidi nilipofuatilia na kuambiwa hakuna kituo chochote cha polisi kinachowashikilia. Nimeelekeza Polisi wafuatilie kwa karibu kujua undani wa tukio hili na hatima yao na kutoa taarifa kwa umma”
 

 

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Komentar untuk "HAYA NDIO MAGIZO ALIOTOA MWIGULU NCHEMBA KWA POLISI KUHUSU SAKATA LA KUTEKWA KWA ROMA"

Back To Top