Profesa Kitila Mkumbo leo amejiuzulu nafasi ya Ushauri wa Chama Cha ACT-Wazalendo mara baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji.
Naye Kiongozi wa ACT, Zitto Kabwe amesema hawawezi kuwanyima watanzania mtu mwenye weledi kwa kuweka maslahi ya chama mbele.
Zitto amesema hayo baada ya mashauriano yaliyofanyika ndani ya chama kufuatia uteuzi huo na kwamba chama cha ACT-Wazalendo kinaunga mkono uteuzi huo.
“Tumeona taarifa ya Rais kumteua Prof. Mkumbo tukaona ni vizuri kufanya mashauri ndani ya chama kwa kuzungumza na Prof.Mkumbo mwenyewe,” amesema Zitto.
Ameongeza kuwa uteuzi huo unaonesha ya kuwa ndani ya vyama vya upinzani kuna watu wenye uwezo na uzalendo wa kutumika katika utumishi wa Umma.
0 Komentar untuk "HAYA NDIO MANENO YA ZITTO KABWE MARA BAADA YA KITILA MKUMBO KUJIUZULU WADHIFA WAKE "