Mahakama
Kuu imemuamuru Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kutotoa ruzuku kwa
Prof. Ibrahim Lipumba wa Chama cha Wananchi, CUF, na kundi lake.
Zuio
hilo ni mpaka shauri dhidi ya Msajili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kuhusu kutoa fedha za ruzuku shilingi milioni 369 kwa njia za wizi na
udanganyifu litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.
Uamuzi huo umefikiwa na Jaji Dyansobela baada ya kukubaliana na hoja zilizowasilishwa kwa hati ya dharura.
Jopo
la Mawakili wa CUF, liliiomba Mahakama Kuu kutoa amri hiyo kwa kuwa
fedha zilizotolewa awali shilingi milioni 369 hazijulikani zimetumika
vipi, na hazikuwa katika mikono salama wala hakuna udhibiti wowote wa
chama kuhusu fedha hizo ikizingatiwa kwamba, Prof. Lipumba alishavuliwa
uanachama.
Mawakili
hao akiwemo Juma Nassor , wamesisitiza kwamba, mazingira yaliyopo ni
vyema na busara kwa fedha za umma zilizopaswa kutolewa kama ruzuku kwa
chama cha CUF kwa sasa ziendelee kubakia serikalini.
0 Komentar untuk "HIVI NDIVYO MAHAKAMA ILIVYOMWAMURU MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUHUSU PROF.LIPUMBA NA KUNDI LAKE"