KAULI YA HAJI MANARA NA ISMAIL RAGE KUFUATIA TFF KUITA KIKAO KUJADILI POINT 3 SIMBA WALIZOPEWA





 Simba spoti klabu ipo kileleni mwa msimu wa ligi kuu Tanzania bara ambapo inaongoza kwa point 62ikiwa na point 6 nyuma yaa watani wao wa amabao ni Yanga huku wakiwa wamesalia na mechi tatu ili kuhitimisha mechi zilizosalia 

Wakati huo huo itakukubukwa kua simba walipewa point tatu na magoli matatu kufuataia kagera suger kumchezea mchezaji wao mohamed fakh ambae inasemaejkana alikua na klazi tatu za jano
wakat hayo yakiendelea nayo timu ya kagera sukari nao hawakukubaliana na matokeo
hayo wakawasilisha barua yao kuomba rufaa hyo iangalie kwa undani kwani wanachokijua mchezaji wao alikua nakadi mbili,
Baada  ya barua hiyo kuwafikia TFF nao wameamua kuitisha kikao kingine amabcho kitakaa kesho ya tarehe 18 siku ya ijumaa nne 
wakati hao yakiwa hivyo msemaji maji wa timu hiyo ya simba Haji manara na Ismail Aden Rage walikua na haya ya kuongea 

Haji Manara, alisema klabu yake inasisitiza kila mwenye haki anatakiwa apatiwe kwa wakati unaofaa na kamwe si kuonyesha viashiria vya TFF kuzipendelea baadhi ya klabu au wanachama wa shirikisho hilo.
 Manara alisema msingi wa kuheshimu vyombo vilivyopo unatakiwa kuheshimiwa huku pia akishangaa kuona Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji inakutana kujadili uamuzi wa rufaa ya Simba wakati Kagera Sugar iliandika barua ya kuomba marejeo.
"Tunaomba haki itendeke, tunatoa tahadhari kuhusiana na kikao hicho, hatuoni uhalali wa kamati hiyo kukutana wakati Kagera Sugar katika barua yake imeomba uamuzi uliotolewa kufanyiwa marejeo, hii inatupa wasiwasi kuna nini hapa," alisema Manara.
Aliongeza kuwa sheria iko wazi inaeleza mtu, taasisi au klabu inapoomba hukumu ifanyiwe marejeo, basi kesi hiyo hupelekwa katika kamati au chombo kile kile na si vinginevyo.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, amewataka viongozi wake kutokaa kimya endapo klabu hiyo itanyang'anywa pointi na kueleza kuwa msingi wa kuheshimu kanuni na sheria ndiyo unatakiwa kufuatwa na si matakwa au kusikiliza presha za upande wowote.

Kanuni ya bodi ya ligi namba 39 (5) (b na c) inaeleza kuwa mamlaka yenye uamuzi wa mwisho kufanya uamuzi ni Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji.
Wakati huo huo ujumbe wa watu watatu wa Kagera Sugar jana ulianza safari kuja jijini kwa ajili ya kuitika wito uliotolewa na TFF wa kuhudhuria kikao cha Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za Wachezaji ambacho pia kitahudhuriwa na watendaji wa Bodi ya Ligi , waamuzi na kamisaa waliochezesha mchezo huo.
Katika kikao hicho, Kagera Sugar itawakilishwa na mratibu wa timu hiyo, Mohammed Hussein, kocha wa makipa na mchezaji Mohammed Fakhi ambaye anadaiwa kucheza akiwa na kadi tatu za njano katika mechi iliyoihusisha timu yake dhidi ya African Lyon.


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Komentar untuk "KAULI YA HAJI MANARA NA ISMAIL RAGE KUFUATIA TFF KUITA KIKAO KUJADILI POINT 3 SIMBA WALIZOPEWA "

Back To Top