KIGOGO CHADEMA AHAMIA CCM,,ANENA HAYA




Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani Tanga, Wilaya ya Muheza, Rwebangira Mathias Karuwasha ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa madai kuwa chama hicho kimepoteza dira na mwelekeo.
Hatua ya kujiuzulu kwake inakuja siku chache baada ya maamuzi wa Mkutano Mkuu wa viongozi wa Chama Kanda ya Kaskazini Mjini Tanga uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe kuridhia kuvunja uongozi wa chama hicho ngazi ya Wilaya ya Mkoa wa Tanga.
Akitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari, Rwebangira Karuwasha amesema hayo ndio mambo makubwa yaliyopelekea kuamua kukaa pembeni na kujiunga na CCM ambako anaona kuna sera makini zinazotekelezeka .
“Lakini kubwa zaidi inatokana na mambo yanayofanywa na chama hicho kwa kuiondoa uhalisi wa chama hicho ambayo wananchi walikuwa wanaitegemea kuwa chama cha kuwa mshindani na CCM ili kuleta mabadiliko,” amesema.
Ameongeza kutokana na matukio mbalimbali anayoyafanya Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe sitegemei kuendelea kubaki kwenye chama hiki cha watumwa na watwana hivyo nimeamua kujiunga na CCM kwani ndio chama kinachoweza kutekeleza sera makini na zenye mafanikio.
“Kwa mfumo wa uongozi unaongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe haukubaliki na hakuweza kuvumilia…. sitegemei kuendele kuwepo kwenye chama hicho kilichokuwa cha watwana na watumwa hivyo nimeridhia kujiunga na CCM,” amefunguka.
“Kuanzia leo mimi sio mwanachama wa Chadema na nitajiunga na CCM ya sasa chini ya Rais, Dokta John Magufuli sababu Chadema wameacha sera makini kwa ajili ya kuwapa maendeleo wananchi,” amesisitiza.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Komentar untuk "KIGOGO CHADEMA AHAMIA CCM,,ANENA HAYA "

Back To Top