Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameamua madaktari wote 258 waliokuwa tayari kwenda kufanya kazi nchini Kenya waajiriwe na Serikali ya Tanzania mara moja.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, ambapo amesema Rais Magufuli amefikia uamuzi huo kutokana na utayari waliouonesha madaktari hao pamoja na wataalamu wengine 11 lakini kwa kuwa kuna pingamizi lililowekwa huko Kenya basi Serikali ya Tanzania itawaajiri wote.
Waziri Ummy Mwalimu alisema kuwa, majina ya Madaktari husika na vituo watakavyopangiwa kazi yatatangazwa katika tovuti ya wizara (www.ehealth.go.tz) pamoja na wataalamu wengine 11 wa Afya waliopeleka maombi yao na kukidhi vigezo
Aidha Waziri Mwalimu amesema Serikali ya Tanzania itakuwa tayari kushughulikia upya ombi la serikali ya Kenya kupatiwa madaktari 500 pale ambapo hakutakuwa na vikwazo vya kupeleka madaktari nchini Kenya
0 Komentar untuk "MADAKTARI WALOKUA WAKITARAJIA KWENDA KUFANYA KAZI KENYA KUAJIRIWA NCHINI TANZANIA- RAISI MAGUFULI"