SOMA MASWALI NA MAJIBU KATIKA KESI YA LISU LEO MAHAKAMANI



Maswali na majibu kati ya shihidi na wakili kibatala kesi ya uchochezi inayomkabili Lissu na wahariri Mawio
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeendelea na usikilizaji wa kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu,
Washitakiwa wengine ni pamoja na Jabir Idrissa Mwandishi mwandamizi wa gazeti la Mawio, Simon Mkina Mhariri wa gazeti la Mawio na Ismail Mahboob Meneja wa kampuni ya uchapishaji magazeti ya Flint.
Leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba upande wa Jamhuri uliowakilishwa na Elia Athanas Rafael Hokolo aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa habari Maelezo ametoa ushahidi.
Tarehe 14 januari walilipokea nakala mbili za gazeti la mawio tolea namba 182.
Tuiona Gazeti la Mawio likiwa limebeba kichwa cha Habari 'Machafuko Yaja Zanzibar'.
Tulipeka taarifa kwa waziri kuwa ni habari yenye uchochozi ili achukue hatua.
Alidai kuwa habari hiyo ilieleza kuwa serikali ya Zanzibar inaongozwa na kufanyiwa na kufanyiwa maamuzi na Serikali ya Tanzania Bara.
Alidai kuwa kuwa habari hiyo ingeweza kuwashawishi wananchi wapinge serikali.
Alidai kuwa baada ya kupeleka taarifa hiyo kwa waziri alichukua hatua.
Amesema kuwa jambo jengine ni kuhusu mchapishaji wa gazeti hilo alikuwa hana kiapo cha kuchapisha gazeti.
Amedai kuwa kiapo kinacho fahamika hapo ni cha Morden News paper printer na sio flint Graphics.
Shahidi alisoma gazeti.
Peter Kibatala wakili upande wa utetezi alimuuliza maswali shahidi juu ya ushahidi alioutoa mahakama hiyo.
Kibatala: nilisikia ukisema kuwa moja ya majukumu yako ni kuwa msemaji wa serikali.
Shahidi: sawa.
Kibatala: kuna uhusiano gani wa kitaasisi kati ya kurugenzi ya mawasiliano Ikulu na Idara ya Habari Maelezo.
Shahidi: kurugenzi ya mawasiliano Ikilu ni wasemaje binafsi wa Shughuli za Rais.
Kibatala: kulingana na kuwa wateule wote wa rais hawawezi kuwa ikulu wewe boss wako ni rais.
Shahidi: ndio.
Ni sahihi kuwa unawajibika chini ya Rais
Shahidi: sahihi.
Kibatala Ni sahihi kwa ushahidi wako wewe habari hiyo ilimtaja Rais kwa jina.
Sahidi IIlimtaja.
KibatalaShahidi kwa ufahamu wako kutajwa kwa Rais na kuhusushwa na machafuko zanzibar. Ni sahihi dhana ya uchochezi unatokana na kutajwa na kuhusishwa kwa Rais
Shahidi: sawa.
kibatala: Rais alipata taarifa ya kufunguwa kwa gazeti.
Shahidi: ndio
Kibatala: Baada ya kufungiwa kwa gazeti muliwahi kupokea mrejesho wowote kutoka Ikulu.
Shahidi : hapana
Kibatala: nilikusikia kuwa wewe ulijiridhisha kuwa habari hii kuwa ni ya uchichozi pekee yako?
Shahidi: hapana tulikaa kikao .
Kibatala:Kulikuwepo kuna Ofisa yoyote wa Jeshi la Polisi kutoka kanda maalumu ya Dar es Salaam.
Kuna Ofisa yoyote wa Jeshi la Polisi aliyekuja kukuhoji.
Shahidi: ndio.
Kibatala: unankumbuka jina au cheo
Shahidi: simkumbuki.
Kibatala: unafahamu chochote kuhusu uuzwaji na usomwaji wa gazeti la Mawio kufungiwa.
Shahidi:Sijui
Kibatala: Ni sahihi kuwa kipengele cha machafuko zanzibar hicho tu. Ndicho kilichosababisha kufungiwa kwa gazeti hilo.
Shahidi: Sahihi
Kibatala: ni sahihi kuwa gazeti la Mawio lilifunguliwa kwa amri ya mahakama ni sahihi kuwa maamuzi ya kufunga gazeti yalikuwa kinyume na sheria.
Shahidi: sijui kwa sababu nimeshastaafu kazi.
Kibatala: gazeti la MwanaHALISI liliwahi kufungwa na kufunguliwa wewe ukiwa kazini ni sahihi kuwa mulikosea.
Shahidi: kimya
Kibatala: Angalia hiyo byline (jina la Mwandishi) ya hiyo stori naonesha ni jina la nani?
Shahidi: Jabiri idrissa
Lakini huku kwenye kesi hakuna mtu anayetuhumiwa kwenye hati ya mashtaka kuna Jabiri Idrissa Yunus
Kibatala: Nimesikia ukizungumzia suala la ripoti hiyo ni nani aliandika hiyo ripoti
Shahidi: Mimi mwenyewe
Kibatala: Kilichopelekea kuandika ripoti yako na kuona kuwa kuana viashiria vya uchochezi ni kichw cha habari au habari ya ndani?
Shahidi: Vyote
Shahidi kuna aya ya tano mwenye kuweza kuzui machafuko haya ni Rais Magufuli kwa kumtangaza mshindi bila hivyo tutarajie umwagikaji wa damu” shahidi alinukuu.
Kibatala: Muliwahi kumuita Jabiri idirisa kabla ya kupeleka ripoti hiyo kwa ajili ya kumuhoji
Shahidi: Hapana nilimpigia simu tu.
Kibatala :Unafahamu kuwa uchaguzi wa marudio wa Zanzibar uliwahi kubashaniwa kisheria
Shahidi: Sijui
Kibatala: Unafahamu kuwa rais aliwahi kusikika akizungumzia matumizi ya vifaru na jeshi kwa atakayepinga uchaguzi huo.
Shahidi: Sikumbuki
Kibatala: Wakati unafanya uchambuzi kwenye gazeti hilo ambalo uliliandika ripoti lissu alihojiwa kama Mwansiasa au Mwanasheria.
Shahidi: kimya
Kibatala: Ni sahihi kuwa Rais wa awamu iliyopita Zanzibar Abeed Amani Karume alishindwa kwenye kinyang’anyiro cha kugombea urais ndani ya CCM na kwamba Gharibu Bilal ndiye aliyeshinda lakini huku walimpitisha Karume
Shahidi: Sijui
Kibatala: Hayo uliyasema kuwa huyafahamu ndio uliyoyaandika kwenye ripoti uliyoipeleka kwa waziri?
Kesi hiyo itaendelea mpaka tarehe 3 Mei mwaka 2017. ambapo shahidi ataendelea kutoa ushahidi.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Komentar untuk "SOMA MASWALI NA MAJIBU KATIKA KESI YA LISU LEO MAHAKAMANI "

Back To Top