UTAFITI:KUTUMIA SIMU GIZANI HUWEZA KUSABABISHA UPOFU





Tafiti zinaonyesha kuwa iwapo mtu atatumia simu janja (smartphone) akiwa gizani (taa ikiwa imezimwa) na akiwa amejilaza kitandani anaweza kupofuka macho.
Imeonekana kuwa utumiaji wa simu janja gizani kwa mfano iwapo taa ikiwa imezimwa na umejilaza kitandani utaweza kupata upofu wa muda (kupoteza uwezo wa kuona kwa hadi dakika 15) na kama utaendeleza sana tabia ya utumiaji huo na usipopata matibabu sahihi unaweza tatizo hilo linaweza likawa ni la kudumu.


Wagonjwa wawili walipatwa na tatizo hilo na baada ya kufanyiwa vipimo vyote ikiwemo kipimo cha moyo na MRI hawakupatikana na tatizo lolote. Walipelekwa kwa mtaalamu wa macho na kuulizwa nini walikuwa wakifanya wakati tatizo hilo likiwatokea na kusema walikuwa wakitumia simu gizani wakiwa wamejilaza kitandani.


Epuka kutumia simu gizani kwa na ukiwa unatumia jicho moja kuangalia
Ugonjwa huo kitaalamu unajulikana kama “ Transient smartphone blindness” ambapo wagonjwa ni watu walikuwa wakitumia simu zao wakiwa wamejilaza kwenye mto jicho moja liikiwa limefunikwa na mto na kutumia jicho moja kuangalia wakati wakitumia simu gizani.
Utumiaji wa simu gizani kusababisha upofu


Daktari alishauri iwapo mtu akiwa anatumia simu gizani atumie macho yote mawili kuangalia kwenye kioo cha simu kwani atakapokuwa anatumia jicho moja na kuacha kutumia simu kisha kutoka kwenye giza, lile jicho ambalo lilikuwa limefunikwa na mto itachukua muda mpaka jicho lile kuweza kuona tena kwani tayari linakuwa limeshazoea giza.

    ASANTE KUENDELEA KUSOMA HABARI KATIKA BLOG HII TAFADHALI LIKE PAGE YETU YA kiraminews KWA TAARIFA MBALI MBALI

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Komentar untuk "UTAFITI:KUTUMIA SIMU GIZANI HUWEZA KUSABABISHA UPOFU "

Back To Top