Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe
amesikitishwa na vitendo walivyofanyiwa wasanii wa muziki Roma Mkatoliki
na wenzake huku akisema hawezi kukubali kuona mambo kama hayo yakiwa
yanaendelea kutokea.
Akizungumza
na wanahabari leo Jijini Dar es Salaam, Waziri huyo amesema
kilichotokea siyo hali ya kawaida kwa watanzania kamwe hawezi
kukubaliana na jambo hilo huku akisisitiza kuwa atafuatilia kwa ukaribu
sana ili aweze kupata majibu ya haraka kabla hajawasilisha bajeti ya
wizara yake
"Hiki
kilichotokea siyo hali ya kawaida kwa watanzania, hatuwezi kukubali
kitu kama hiki kiendelee kutokea,nitalifuatilia kwa ukaribu sana,
nitajitahidi nipate majibu kabla ya bajeti yangu Bungeni". Alisema Dk. Mwakyembe
Hata
hivyo Dkt. Mwakyembe amewataka wananchi waache tabia ya kuamini kila
maneno yanayosemwa na watu ambao hawana ujuzi katika masuala ya
uchunguzi, hivyo wanapaswa kuvipa muda vyombo vya dola viweze kufanya
kazi zake kwa ufasaha.
"Nilishasema kuwa nimeagiza vyombo vya dola vifanye uchunguzi
ili ajulikane aliyewafanyia hivi wakina Roma kama ni nani kama wa dola
ntadili naye, tuache uchunguzi ufanyike, tuache kupiga ramli". Alisisitiza Mwakyembe
Pia Waziri huyo mwenye dhamana na wasanii ametoa ujumbe kwa vyombo
vyote vilivyopo chini ya Wizara yake kutofanya mahojiano yoyote
yanayowahusu wasanii hao bila ya kuwepo taarifa kamili kutoka kwake.
Kwa
upande mwingine Roma ambaye ambaye amesimulia tukio lilivyokuwa amesema
kwa sasa hawezi kuongea mambo mengi kwa kuwa kila kitu amekwisharipoti
polisi kila kitu, na kwamba kuna mambo akiyaweka hadharani atakuwa
anaingilia upelelezi wa polisi.
Pia
amesema hawezi kujua kama kweli tukio hilo lililowatokea linahusiana
na muziki kwa kuwa ameweza kuhusishwa mpaka mfanyakazi wao wa ndani
ambaye hana hata chembechembe za uimbaji.
0 Komentar untuk "WAZIRI MWAKYEMBE AAHIDI KUWAKAMATA WALIOWATEKA WAKINA ROMA"