Mabingwa watetezi wa Tanzania Bara Yanga SC wamesema hawana imani na kamati iliyoundwa ya saa 72 ya kuchunguza rufaa ya Simba SC kwa Kagera Sugar kwa kuwa imeshaanza mipango ya kuchakachua ripoti ya mwamuzi kwa lengo la kusaka ushindi wa mezani.
Hayo
yameibuliwa na Katibu Mkuu wa Yanga SC pamoja na wajumbe wa kamati yake
ya utendaji ikiongozwa na Salum Mkemi kwa kusema haitakuwa jambo la
rahisi kwa kupata haki ya ukweli kwa kile kinachoonekana ndani ya kamati
hiyo kujaa maslahi binafsi badala ya kulinda heshima ya ligi.
"Kamati hii imechelewa kutoa
maamuzi kwa kuandaa ripoti za uongo za michezo dhidi ya Fakhi pia tuna
taarifa za kughushiwa barua pepe (email) na nyaraka nyingine, ili kuipa
alama tatu Simba SC yenye zaidi ya wajumbe 6 ndani ya kamati hiyo.
Tumeshavijulisha vyombo husika yaani TAKUKURU na watu wa 'Cyber
Crime' na TCRA juu ya uchunguzi wa mawasilano ya waamuzi wote
waliohusika na kutajwa kwenye rufaa hiyo". Alisema Mkemi pindi alipokuwa anaongea na wanahabari katika ukumbi wa klabu hiyo, Jangwani jijini Dar es Salaam
Vile vile mjumbe huyo ameendelea
kubainisha baadhi ya vitu kwa kusema wameshaanza kufanya uchunguzi wao
na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola huku wakijipanga kwenda mahakamani
endapo wapinzani wao watabebwa kwa namna moja ama nyingine.
"Kama
Yanga tumeanza uchunguzi wetu na kutoa taarifa kwa vyombo husika vya
dola pia maamuzi yoyote ya kuibeba Simba tutakwenda mahakamani licha ya
sheria za FIFA kukataza hivyo kama hawataki tufike huko lazima haki
itendeke". Amesisitiza Mkemi
Hata hivyo klabu hiyo imetoa rai yao
kuwa ifike wakati ziundwe kamati zisizokuwa na maslahi pande yoyote ile
ili kuleta haki katika maamuzi mbalimbali y soka nchini.
Kwa upande mwingine imewapongeza timu ya
Simba SC kwa ushindi wao wa jana dhidi ya Mbao FC kwa kuonesha
kupambana na kuweza kurudisha magoli yote mawili na kushinda mechi
0 Komentar untuk "YANGA SC YAAHIDI KWENDA MAHAKAMANI ENDAPO HAKI HAITOTENDEKA KATIKA RUFAA YA POINT TATU YA KAGERA NA SIMBA "