Mbunge wa Kigoma mjini kupitia tiketi ya ACT, Zitto Kabwe ameukosoa mpango wa serikali kuanza kujenga reli ya kati baina ya Dar es Salaam na Morogoro na kusema serikali inapaswa kuangalia vipaumbele vya maeneo ambayo shughuli za reli hiyo itasaidia
Zitto
amebainisha hayo wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano katika mkutano wa Bunge Jijini Dodoma kwa kumtaka Waziri
Profesa Makame Mbarawa aangalie takwimu ni wapi anapaswa apeleke reli
ili aweze kupata pesa ya kujenga reli nyingine.
"Toka
mwaka jana tumelalamika kuhusu jambo hili...Nawashukuru wabunge
wemametoa tafsiri mpya ya reli ya kati, reli ya kati tafsiri yake ni
Kigoma Dar es salaam au Dar es salaam Kigoma maeneo mengine yote ni
matawi ya reli ya kati......
"Lakini
ujenzi wa 'Standard Gauge' kwa hatua hizo wanazoziita za awali unatoka
Dar es salaam kwenda Mwanza....Namuomba Waziri aangalie takwimu ni wapi
atapeleka reli ili apate pesa ya kujenga reli nyingine.......
"Takwimu
zinaonesha kwamba mizigo ambayo Tanzania inahudumia kwa nchi za maziwa
makuu ni tani Milioni tano kwa mwaka kwa mujibu taarifa ya hali ya
uchumi mwaka 2015/2016.
"Katika hizo asilimia 34 ni Zambia, asilimia 34 ni Kongo, asilimia 12 Rwanda, aslimia 6 Burundi, asilimia 2.6 Uganda...
"Unapoanza
na 'Standard Gauge' matailion ya fedha ukaipeleka Isaka na Mwanza maana
yake ni kwamba unaenda kuhudumia mizigo aslimia 15 ya mizigo yote
tunayoipitisha unaacha kwenda kuhudumia mizigo asilimia 40 kwa maana ya
Kongo na Burundi ambayo yote inapita Kigoma". Alisema Zitto
Aidha,
Zitto amehoji wizara pamoja na serikali kuwa ni njia gani walizozitama
mpaka kuamua kupeleka sehemu ambayo wanajua haiwezi kuleta faida kwa
taifa.
"Economics' gani ambazo mmetumia katika kuhakikisha kwamba reli inaelekea mahali ambako hakuna mzigo..
"Sipendi
kusema kwamba Kigoma inatengwa siyo lugha ambayo mimi kiongozi napenda
kuzungumza lakini hili takwimu zote zinaonesha reli inapaswa kwenda
kule ambako kuna faida, hampeleki kule ambako kuna faida ambako kuna
faida hii maana yake nini ?...
"Lakini
siyo hivyo tu Waziri, kuna fedha za Benki ya Dunia ...kwaajili ya
ukarabati wa reli hata hizi Bilioni 200 za ukarabati wa reli ambao upo
sahizi na zenyewe mmepeleka kule kule mnapopeleka 'Standard Gauge',
mnashindwa hata kutudanganya kwa pipi". Alihoji Z
0 Komentar untuk "ZITTO-ECONOMICS GANI MMEITUMIA KUIPELEKA RELI MAHALA AMBAKO HAKUNA MIZIGO?,SOMA ALIVYOIKOSOA SERIKALI "