TAARIFA
KWA UMMA KUHUSU WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2017 WANAOKUSUDIA
KUOMBA KUJIENDELEZA KATIKA NGAZI YA CHETI AU STASHAHADA KATIKA VYUO
VINAVYOSIMAMIWA NA BARAZA KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018
Baraza
linapenda kuwataarifu wahitimu wa kidato cha sita waliohitimu mwezi Mei,
2017 na umma kwa ujumla; kuwa sasa wanaweza kutuma maombi ya Udahili
wa kozi za Afya na Ualimu katika Vyuo vya Serikali kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) au kupitia vyuo husika vya Afya na Ualimu ambavyo vitashughulikia maombi hayo na kufanya Udahili kwa njia ya mtandao kupitia ‘Institutional Panel’ zao.
Kwa wale
ambao walishatuma maombi na wanataka kuongeza sifa ya kidato cha sita
wanaweza kufanya hivyo sasa kupitia kurasa zao binafisi (Profile).Pia
baraza linapenda kuwakumbusha na kuwahimiza wote wenye sifa kama zilivyo
ainishwa kwenye kitabu cha Muongozo wa Udahili (Admission Guidebook)
kinachopatikana kwenye tovuti ya Baraza kuwa, wafanye maombi yao mapema
kabla ya tarehe 20 Agosti, 2017 kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza kwa
sababu hakutakuwa na muda wa nyongeza.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 22/07/2017
0 Komentar untuk "NACTE WATOA TAARIFA MUHIMU KWA KIDATO CHA SITA WALIOMALIZA MWAKA HUU 2017"