Mkurugenzi mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba anapenda kuwatangazia wananchi wote
nafasi za kazi kwa kada mbalimbali kama ifuatavyo hapa chini
DEREVA: NAFASI 1
MAJUKUMU
i. Kuendesha magari ya abiria na malori
ii. Kuhakikisha
gari na vyombo vyake vipoo katika hali nzuri wakati wote na kufanya
uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji
matengenezo
iii. Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari
iv. Kutunza na kuandika daftrai la safari LOG – BOOK kwa safari zote
SIFA ZA MWOMBAJI
i. Awe na elimu ya kidato cha 4 au 6
ii. Mwenye lesseni ya daraja “C” pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mi 3 bila kupata ajali
iii. Mwenye cheti cha majaribio ya ufundi daraja la II
iv. Mwombaji asiwe na umri unaozid miaka 45
N
GAZI YA MSHAHARA TGOS A
DEREVA MASHUA/KIVUKO DARAJA LA II - NAFAI I
MAJUKUMU
- Kufunga na kufungua kamba za mashua
- Kuchunga usalama wa abiria na magari yaliyomo ndani ya kivuko
- Kupanga abiria na magari ndani ya kivuko
- Kuendesha na kuongoza kivuko
- Kutunza daftari la safari za kivuko
- Kuhakiki kuwa inijini za kivuko zipo katika hali nzuri ya kufanya kazi
- Kuangalia mafuta na vyombo vingine vya kufanyia kazi
SIFA ZA MWOMBAJI
- Awe na elimu ya kidato cha 4 au 6
- Awe na ujuzi wa
kuendesha na kutunza kivuko uliothibitishwa na chuo cha DSM MARINE
INSTITUTE na chuo kingine kinachotambuliwa na serikali kwa muda
usiopungua miaka miwili
- Awe amefuzu mafunzo ya miezi 6 ya uokoaji wa maisha majini , kuogelea na kupanga watu na magari kwenye kivuko
NGAZI YA MSHAHARA TGOS A
KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III NAFASI 1
MAJUKUMU
a. Kuchapa barua , nyaraka na taarifa za kawaida
b. Kusaidia kupokea wageni, kuwasaili shida zo na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa
c. Kusaidia kutunza
taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za mkuu
wake na ratiba yake ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika
ofisi anayofanyia kazi na kumuarifu mkuu wake kwa wakati unaohitajika
d. Kusaidia kutafuta na kumpatia mkuu wake majalada , nyaraka au chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini
e. Kusaidia
kufikisha maelezo ya mkuu wake wakazi kwa wasaidizi wake na pia
kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi wao
f. Kusaidia
kuyapokea majalada na kuyagawa kwa maofisa walio katika sehemu alipo
na kuyakusanya , kuyatunza na kuyarudisha sehemu husika
g. Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na msaidizi wake wa kazi
SIFA ZA MWOWOMBAJI
a.
Awe na elimu ya kidato cha 4 au 6
b. Awe amehitimu
mafunzo ya uhazili na kufahulu hatua ya 3 ya somo la hatimkato la
Kiswahili na kingereza maneno 80 kwa dakika moja
c. Awe amepta
mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali
na kupata cheti katika program za windows Ms Office, internet,
E-mail na Publisher
d. Mwombaji asiwe na umri uliozod miaka 45
NGAZI YA MSHAHARA TGS B
MSAIDIZI WA KUMBU KUMBU DARAJA LA II NAFASI 1
MAJUKUMU
• Kutafuta kumbukumbu/nyaraka /mafaili yanayohitajika na wasomaji
• Kuthibiti upokeaji na uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka
• Kuchambua ,
kuorodhesha na kupanga kumbukumbu /nyaraka katika makundi kulinganna na
somo husika kwaajili ya matumizi ya ofisi
• Kuweka na kupanga kumbukumbu / nyaraka katika reki/file racks cabinet katika masijala
• Kuweka barua/kumbukumbu katika mafaili
• Kuchambua na kutafsiri kumbukumbu kwaajili ya mipango na huduma za ofisi
• Kutunza/kudhibiti na kutoa kumbukumbu za halmashauri
SIFA ZA MWOMBAJI
• Awe na elimu ya kidato cha 4 au cha 6
• Awe amefuzu mafunzo ya cheti cha utunzaji kumbukumbu katika moja wapo ya fani za afya, masijala, mahakama na ardhi
• Mwombaji awe na umri usiopungua miaka 45
NGAZI YA MSHAHARA TGS B
MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III NAFASI - 4
MAJUKUMU
i. Afisa msuluhishi na mtendaji mkuu wa Serikali ya kijiji
ii. Kusimamia ulinzi na usalma wa raia na mali zao kuwa mlinzi wa Amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji
iii. Kuratibu na usimamia upangaji wa maendelo ya kijiji kuratibu mikutano ya kamati zote za Halmashauri ya kijiji
iv. Kutafsiri na kusimamia sera, sharia na taratibu
v. Kusimamia, kukusanya, na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji
vi. Mwenye wa kikao ch wataalamu walipo katika kijiji
vii. Kupokea, kusikiliza, na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi
viii. Kusimamia utungaji wa sharia ndogo za kijiji
ix. Atawajibika kwa mtendaji wa kata
SIFA ZA MWOMBAJI
i. Awe na elimu ya kidato cha 4 au 6
ii. Awe amehitmuu
mafunzo ya stashahada ya cheti katika moja ya fani zifuatazo utawala,
elimu ya jamii, sharia, usimamizi wa fedha, maendeleo ya jamii, na
sayansi ya Sanaa kutoka chuo kikuu Hombolo au chuo chochote
kinachotambulika na serikali
iii. Mwombaji asiwe na umri chini ya miaka 45
NGAZI YA MSHAHARA TGS B
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Barua za maombi ziandikwe kwa mkono
Barua ziandikwe kwa
MKURUGENZI MTENDAJI WILAYA,
HALMASHAURI YA WILAYA,
S.L.P 131
MULEBA
Muombaji aambatanishe
- CV, yenye namba za simu za kuaminika na wwadhamini watatu wa kuaminika
- Nakala za vyeti vya elimu ya sekondari na chuo
- Hati ya kuzaliwa
- Leseni ya udereva kwa watakao omba udereva
- Picha moja ya passport size
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
- Waombaji wawe raia wa Tanzania
- Barua za uthibitisho wa matokeo ya mithani result slip na tesmonials procisional hazitapokelewa
- Wale ambao ni watumishi wa barua zao maombi zipitie kwa waajiri wao
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa TCU NA NECTA
- Waombaji
waliotaifishwa katika utumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
kama wanakibali cha utumishi wa katibu mkuu kiongozi
- Uwasilishaji wa taarifa za kughushi ni wahusika watachukuliwa hatua za kisheria
- Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 09/09/2017
0 Komentar untuk "NAFASI ZA KAZI/ AJIRA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MULEBA"