Mambo ya msingi na lazima unapokua unajibu maswali katika usahili
Si kwamba wanaokoswa ajira baada ya usahili(interview) hawana majibu sahihi.Hili si kweli ukweli uliopo ni kuwa mtu anaingia kwenye usahili pasipo kujua ni namna gani anaweza kujibu maswali hivyo huishia kukoswa ajira ambayo ilikuwa ni stahiki yake kabisa. Haya hapa ni mambo matatu ya kuzingatia wakati unapoingia katika chumba cha usahili na kuanza kujibu maswali hakika ikiyazingatia wewe hautakuwa wa kushindwa usahili kila mara.
1. Zungumza taratibu na kwa uhakika.( speak slowly and clearly)
Unapojibu swali inakupasa ujibu kwa sauti ya kawaida na kwa uhakika hii itaonesha ni jinsi gani unaelewa kile unachosema.Pia unapoongea kwa taratibu itakuwa rahisi kwako kuweza kupangilia mawazo yako vema.Wengi wamekoswa ajira kwa sababu ya kuongea kwa haraka na kupelekea kushindwa kueleweka wanachosema.
2. Weka kituo kabla hujaanza kujibu swali.(Pause slightly before you begin)
Unapoulizwa swali hakiksha unafikiria kabla ya kujibu hili uwe na majibu sahihi.Sina maana ukae muda mrefu unafikiria jibu hii nayo si nzuri,hapa cha kuzingatia ni kuwa na mwanzo mzuri wa kujibu wenye tafakari ya uhakika kuliko kujibu wakati hata hujui unajibu nini
3. Andaa majibu kwa baadhi ya maswali ya msingi(Prepare answers to some basic questions)
Maswali ya msingi hutokana na jinsi nafasi unayoomba hivyo ni vizuri ukawa na majibu hayo mapema ili unapoulizwa usitumie muda mwingi kufikiria,pia utajibu kwa uhakika kwa sababu majibu umeyazoea tayari.Kumbuka kuwa makini na kile ulichoandika katika barua yako ya maombi na taarifa za kwenye “CV” yako.Wengi wamekoswa ajira kwa kuandika vitu katika “CV” zao na wanashindwa kuvieleza.
0 Komentar untuk "MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOKUA UNAJIBU MASWALI KATIKA USAHILI"