HARRISON Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ana mambo mengi ya kufanya kwa sasa, lakini siyo ripoti ya mtangulizi wake, Nape Nnauye,
Uteuzi wa Nape ulitenguliwa akiwa anatarajia kukabidhi ripoti ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kudaiwa kuvamia kituo cha Clouds Media.
Waziri Mwakyembe amesema hawezi kutoka na kauli za papara na matamko ya haraka haraka ambayo yanaweza kuleta matatizo siku za mbele.
Alisema ripoti ya Nape dhidi ya Makonda siyo kipaumbele kwake bali yapo mambo mengi ya muhimu ya kufanya badala ya kuhangaika na jambo hilo ambalo halijakamilika kisheria. “Nimekuwa naulizwa sana na waandishi wakati naapishwa. Kwanza hiyo ripoti yenyewe sijaiona, lakini hata nikiiona siwezi kuipeleka kwani haijakamilika, maana imehoji upande mmoja,” amesema Mwakyembe.
Mwakyembe amesema akiwa kama mwanasheria kwa mujibu wa ibara ya 13 ibara ndogo ya sita (a) na sheria ya jumla anaheshimu sana kanuni hivyo kitu chochote lazima kiheshimu katiba na haki kwani mtu hawezi kuwa hakimu katika suala lake mwenyewe.
Akizungumzia kuhusu kuboresha wizara yake, amesema atahakikisha anafanya kazi kwa karibu na watendaji wake ili kuifanya wizara hiyo kuwa na maendeleo ya haraka.
Amesema kuna mambo mengi ambayo hatahaikisha anayafanya ikiwa ni pamoja na kuhunganisha wasanii ili kuondokana na tofauti zao na badala yake waunganishe nguvu ya kufanya kazi zao.
Pia Mwakyembe amesema atashughulikia usimamizi wa umaliziaji wa sera ya sanaa na filamu ikiwa ni pamoja na kupambana na mahalamia wa wizi wa kazi za wasanii.
0 Komentar untuk "RIPOTI YA NAPE SIO KIPAUMBELE KWANGU:WAZIRI MWAKYEMBE"