Serikali
imesema jumla ya walimu 3,081 wakiwemo walimu 7 wa shule ya Sekondari
Omumwani Kagera, wameajiriwa, hivyo bado kuna nafasi ya walimu 1.048
kati ya nafasi 4,129 za walimu wa Sayansi na Hisabati zilizotolewa
kibali cha ajira.
Taarifa
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa akizungumza
na Waandishi Habari,ofsini kwake ambapo amewataka walimu wote
walioajiriwa wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kuanzia
tarehe 18 hadi 25 mwezi huu.
Amesema
walimu walioajiriwa wamepangwa moja kwa moja na TAMISEMI katika
halmashauri zote nchini ambazo zina upugufu wa walimu wa Sayansi na
Hisabati.
Simbachawene amesema kati ya walimu hao walioajairiwa walimu 1,537 ni wa Shahada na walimu 1,544 ni wa Stashahada.
“Sehemu
kubwa ya walimu wa Shahada wamepangwa kwenye shule za kidato cha tano
na sita na wachache kwenye shule za kidato cha kwanza hadi cha nne’’
alisema.
Simbachawene
amekiri kuwa kuna upungufu wa walimu 26,026 wa masomo Sayansi na
Hisabati katika shule mbalimbali za sekondari nchini.
“Moja
ya changamoto kubwa ambazo zinaikabili sekta ndogo ya elimu ya
sekondari ni upungufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati upungufu uliopo
katika shule 3,602 ni 26,026 sawa na asilimia 60.14 ya walimu 43,248
wanaohitajika” amesema Simbachawene
0 Komentar untuk "BREAKING NEWS :SERIKALI YATOA AJIRA KWA WALIMU 3,081, WALIMU HAO WANAHITAJIKA KURIPOTI TAREHE 18 HADI 25 MWEZI HUU."