Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli amepokea barua yenye ujumbe wa Rais wa Jamhuri wa Rwanda Mhe. Paul Kagame iliyowasilishwa kwake na Mjumbe Maalum ambaye ni Waziri wa Elimu wa Rwanda Dkt. Musafiri Papias Malimba.
Pamoja na kupokea barua hiyo, Mhe. Rais
Magufuli na Dkt. Musafiri Papias Malimba wamezungumzia masuala
mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda ikiwemo katika
sekta ya elimu hususani maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza
Rwanda kwa kuamua lugha ya Kiswahili ianze kufundishwa katika shule zake
na ameahidi kuwa Tanzania ipo tayari kutoa walimu wa kwenda kufundisha
lugha hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Dkt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda na Mjumbe maalumu wa Rais Paul Kagame alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 20, 2017. Wengine ni Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Kayihura na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi Bw. Issa Mugabutsinze.
0 Komentar untuk "HABARI NJEMA KWA WALIMU WALIOSOMA KISWAHILI SASA KWENDA KUFANYA KAZI NCHINI RWANDA "