HAYA NDIO ALIOYAONGEA NAPE NNAUYE JIMBONI KWAKE HII LEO



Leo jumamosi ya april 8 mmbunge wa jimbo la mtama muheshimiwa NAPE NNAUYE aliahidi kuongea kilichotoea wakati anavuliwa uwaziri wake na haya ni baadhi ya maneno alioongea leo hii akiwa jimboni kwake yapo hapa 

nilitaka kuongea nikiwa Daresalama ikatokea fujo hivyo nimeamua nije kuongea huku kwangu mtama
siku ile nilivyofika kwa ajili ya kuongea na waandishi wa habari yule kijana mpuuzi mliemuona akasogea karibu yangu  ikabidi nikamnongoneza tuko moja kwa moja vyombo vya habari vinaangalia ,
Pindi aliponyosha bastola nilitaka kumwambia na mimi ninakubwa zaidi yako lakini nikaona sote tutakua wapuuzi
Matendo haya yanachonganisha CCM na wananchi,huko mtaani watu wanasema nimshauri Raisi kama mwenyekiti wa chama changu,
Mimi nimewasemehe ila haya matendo mengine yanamjengea chuki yeye (Raisi)kwa wannchi wakidhani ni yeye ndie anaewatuma

kazi ya msingi ya kikatiba ya serikali ni kulinda raia .Namuomba Raisi aunde tume huru ichunguze matendo haya yasijirudie tena

Kijana mmoja wa CHADEMA BEN SAANANE amepotea kwa miezi mingi ,watu wamevamia kituo na vyombo vya usalama wameonekana

Niamini kama alitumwa ,mimi ukinitolea silaha naona kama MIC tu,shida nilionayo ni vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya nini?
Na nilisubiri wamtafute yule kijana alioninyeshea bastola  lakini wamesema sio polisi lakini wewe leo nyoosha bastola hewani uone kama hawajaondoka na wewe

Nilikasirika na amiini mtanisamehe kwa kukasirika kwangu  kwani na mimi ni mwanaadam na nina nyongo hivyo nilikumbunga mengi saana 
Katika sakata hilo kuna mambo ya kipuuzi saana yaliotokea ,kwanza walisema  mtandaoni kua nimekamatwa na mimi nikaandika kua sijakatwa walipoona hivyo wakaamua kwenda kuwaondoa waandishi hotelini nilikuaa  nimepanga kufanya kikao changu na waandishi wa habari
kwakua kocha kaamua hakuna haja ya kumnunia lakini pale mechi  itakapokua ngumunitarudishwa uwanjani kwani mimi ni mchezaji bora
Wakati mwingine ukiwa mchezaji mahairi na ukafunga  magoli ya kutosha ina bidi umpimzishe ili acheze kesho
Na karatasi ya utenguzi wa uwaziri wangu ukiisoma hakuana sababu ya bali yalikua ni matakwa ya raisi
Namshukuru Raisi amabe nilipambana kufa na kupona kuhakikisha anakua Rais hadi kupata ajali mbaya wakat natoka kutafuta kura 
Nilifanya kazi nzuri sana kuhakikisha dhamana niliopewa nimeifanyia haki na kama yupo mtu anadai sikutenda haki asimame hadaharani aongee


Share :

Facebook Twitter Google+
0 Komentar untuk "HAYA NDIO ALIOYAONGEA NAPE NNAUYE JIMBONI KWAKE HII LEO"

Back To Top