Rais Magufuli amezindua Rasmi ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa ya Kimataifa ambayo treni ya kisasa inayotumia umeme itaweza kusafiri kwa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa.
Hizi ni baadhi ya sentesi 20 alizoongea
21.Unapokuwa
dereva wa lori na unapopakia abiria hutakiwi kuwauliza wasimame
waangalie sehemu gani, dereva mzuri anangalia kufika salama
20.Niwaombe
tuangalie TZ kwanza siasa baadae, muiache Serikali ya CCM iliyoaminiwa
na Watanzania itekeleze wajibu wake tutakutana 2020
19.Watanzania wanataka maendeleo, hakuna anayekula siasa kwa hiyo Tanzania kwanza siasa baadae
18.Tanzania tunaweza kwa hiyo tunapoyafanya haya tunafanya kwa sababu tuna wajibu wa kufanya, na haya ni malipo yangu kwenu
17.Niko kwa niaba yenu, tumeonewa sana, Tanzania ni tajiri hatutakiwi kuwa ombaomba
16.Mlinituma nifanye haya, au niwaulize ndugu zangu haya yote ninayoyafanya kweli ni mabaya?
15.Nazuia
hata michanga ya madini, ninafanya kazi hii kwa niaba yenu, kwani
nashindwa kusema nipelekee hiyo michanga nitaikuta Ulaya?
14.Wanasema
samaki mkunje akiwa mbichi, fisadi mkunje akiwa mbichi akishakomaa
mvunje, nafuu walalamike wachache, Watanzania wafurahi
13.Vita ya kupambana na ufisadi ni ngumu na hasa unapowabadilisha watu wachache waliozoea maisha fulani kwa miaka 50
12.Nataka mhandisi amalize mradi wa reli ya kisasa kabla ya miezi 30, na ikiwezekana siku ya kufungua twende bure mpaka Dodoma
11.Tunajua tunapoenda pasitokee mtu wa kubadilisha ajenda tuanze kuzungumzia ajenda ambazo hazipo kwenye ilani ya uchaguzi
10.Hivi karibuni tumepata mkopo wa kuanza kujenga barabara za mwendokasi katika awamu ya tatu na ya nne
9.Tanzania imekuwa kwa uchumi 7%, ushahidi wa kukua kwa uchumi ndio hii miundombinu tunayoijenga
8.Kazi
tunazozifanya mara nyingi utakaowaona wanapiga kelele ni wale ambao
walizoea kupiga dili, na mimi nataka waendelee kupiga kelele
7.Nawahakikishia Watanzania mimi ni dereva mzuri nawahakikishia lori litafika kule tunakokwenda na hili ni lori la maendeleo
6.Wale
wataalamu wa kusoma kwenye mitandao wakaangalie ni nchi gani imejenga
reli ya namna hii kwa pesa zake watakuta ni Tanzania
5.Mradi huu wa ujenzi wa reli ya kisasa unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 30
4.Mradi huu wa ujenzi wa reli ya kisasa unatarajiwa kutoa ajira kwa watu takribani 600,000
3.Ujenzi
wa reli hii ya kisasa utasaidia kutunza barabara zetu, barabara zetu
zinaharibika kwa sababu zinasafirisha mizigo mikubwa
2.Ujenzi
wa reli ya kisasa utakuza sekta zingine nchini, itawezesha malighafi
mbalimbali kusafirishwa kwenda kwenye maeneo ya viwanda
AHSANTE KUENDELEA KUSOMA HABARI KATIKA BLOG YETU
ILI KUPATA HABARI KWA WEPESI ZAIDI LIKE PAGE YETU YA kiraminews
IPO UPANDE WA JUU WA KUSHOTO WA BLOG HII
0 Komentar untuk "HAZI NI SENTESI 20 MUHIMU ALIZOZIONGEA RAISI MAGUFULI LEO KATAKA UZINDUZI WA RELI YA KISASA "