HII NDO KAULI YA MWIGULU NCHEMBA MARA BAADA YA KUFIKA WALIPOUAWA ASKARI POLISI




WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi,Mwigulu Nchemba,amesema hawatokubaliana na mtandao,kundi ama mtu anaehusika na kugharimu maisha ya askari ama wananchi wasio na hatia.

Aidha amebainisha kwamba kilichombele kwa sasa ,wanaendelea kuhakikisha kuwa wanarudisha silaha zinazochukuliwa katika matukio mbalimbali ya mauaji ya askari na kuendelea na mapambano na wahalifu hao.

Nchemba ameyasema hayo jana  ,wilayani Kibiti,mkoani Pwani,na kumtaka mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo kupambana na matukio ya mauaji yanayoendelea katika baadhi ya wilaya mkoani hapo.

Waziri huyo wa mambo ya ndani ,alieleza kwamba,amepokea taarifa ya kuuwawa kwa askari nane wilayani Kibiti  kwa mshituko mkubwa .

Nchemba aliwaomba watanzania kwa kipindi hiki wawe watulivu wakati jeshi la polisi likiendelea kukabiliana na mambo hayo.

Hii ni changamoto kwa wizara ya mambo ya ndani kuanza upya kuboresha mbinu zake za ki intelensia zinazoendana na mazingira ya sasa kwa mahitaji ya sasa”alisema.

Alibainisha kwamba,ni ngumu kuingia akili kwa watu wachache kuuwa hovyo askari ambao ndio walinzi wa raia na mali zao

Kuna jambo lipo nyuma limejificha ambalo mwisho wake umefika kwani hatutoweza kulifumbia machoalisisitiza.

Nchemba aliomba jamii iendelee kulinda amani ya nchi na kuheshimu askari polisi ambao wapo kwa ajili ya kuwalinda katika usalama wao.
 
 AHSANTE KUENDELEA KUSOMA HABARI KATIKA BLOG YETU 
ILI KUPATA HABARI KWA WEPESI ZAIDI LIKE PAGE YETU YA kiraminews
 IPO UPANDE WA CHINI NA UPANDE WA JUU WA KUSHOTO  WA BLOG HII
 

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Komentar untuk "HII NDO KAULI YA MWIGULU NCHEMBA MARA BAADA YA KUFIKA WALIPOUAWA ASKARI POLISI"

Back To Top