HII NDO TAARIFA SAHIHI KUFUATIA HABARI YA SIMBA KUPEWA POINT TATU ZA KAGERA




Wakati taarifa zimekuwa zikisambaa mitandaoni kuwa tayari Simba to
wameshinda rufaa yao na kupewa pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar, ukweli ni kwamba kikao cha kamati ya Saa 72, kitakaa saa 9 Alasiri jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho kitakaa leo hii na kuamua kuhusiana na rufaa hiyo ya Simba inayolalamika mchezaji Mohamed Fakhi kuwa na kadi tatu za njano.
Katika mechi hiyo iliyopigwa mjini Bukoba, Simba ililala kwa mabao 2-1.
Lakini kuanzia muda mchache uliopita, taarifa zimekuwa zikisambaa mtandaoni kwamba tayari kikao kimekaa na Simba wamepewa pointi tatu.
"Kikao bado, itakuwa saa 9, hao wanaosema nafikiri wanazusha tu mambo," alisema mjumbe mmoja wa kamati hiyo.
"Watuache tufanye kazi yetu, wasilazimishe mambo na kutaka kuleta mkanganyiko."

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Komentar untuk "HII NDO TAARIFA SAHIHI KUFUATIA HABARI YA SIMBA KUPEWA POINT TATU ZA KAGERA "

Back To Top