Kamishna
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Simon Sirro amesema kuwa
tayari wameshapata taarifa za kupotea kwa Msanii wa Bongo Fleva hapa
nchini, ‘Ibrahim Mussa’ maarufu kwa jina la Roma Mkatoliki na kuongeza
kuwa tayari timu yake ya upelelezi imeshaanza kazi.
Ameyasema
hayo mapema hii leo wakati akizungumza na Katibu wa Chama cha Wanamziki
wa Kizazi Kipya Tanzania, Samweli Mbwana alipotaka kujua kama Jeshi la
Polisi lina taarifa ya kupotea kwa mwanamziki huyo.
Sirro
amesema kuwa taarifa za kupotea kwa msanii huyo tayari wameshazipata na
Jalada la upelelezi tayari limeshafunguliwa kwa ajili ya upelelezi.
Ameongeza
kuwa timu yake ya upelelezi iko mtaani kwa ajili ya kujua
kinachoendelea, na amewaomba wasanii na baadhi ya watu kutokuwa wepesi
wa kusambaza uvumi usiokuwa na ukweli ndani yake.
“Jamani
mambo ya uvumi yaacheni, sio kitu kizuri unamvumishia mtu kitu ambacho
hakijui na wengine wanasema kuwa Serikali inahusika kitu ambacho si cha
kweli”,amesema Kamanda Sirro.
Aidha,
Sirro amesema kuwa amepanga kukutana Waandishi wa Habari kesho saa tano
Ofisini kwake ili kuweza kutoa ripoti kamili kuhusu kupotea kwa msanii
huyo wa Bongo fleva kwani timu ya upelelezi tayari iko kazini.
Hata
hivyo, amewatoa hofu wasanii na wananchi kwa ujumla kwamba suala hilo
linafanyiwa kazi, hivyo hakuna haja ya kuogopa na kuendelea kuvumisha
vitu visivyokuwa vya msingi.
0 Komentar untuk "KAMANDA SIRRO ANENA MAZITO KUHUSU SAKATA LA KUPOTEA KWA "ROMA" "