KIKWETE ASHANGILIWA KWA ZAIDI YA DAKIKA KUMI ALIPOINGIA BUNGENI LEO



Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo ameshangiliwa kwa muda wa zaidi ya dakika kumi (10) mara baada ya kuingia bungeni na kutambulishwa leo asubuhi.
Shangwe hizo ziliibuka kutoka kwa wabunge wote wa Chama Tawala CCM na wale wa upinzani ambapo kwa umoja wao wamemshangilia vilivyo mstaafu huyo.
Kutokana na hali hiyo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amekiri kuwa haijawahi kutokea mgeni kushangiliwa kwa muda mrefu kwa kipindi chote alichokuwepo bungeni.
Bunge limeanza leo Mjini Dodoma ambapo kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ukitarajiwa kufanyika leo saa 7:00 mchana baada ya vyama vyote kuwasilisha nyaraka muhimu.
Wakati huohuo, Mbunge wa Kuteuliwa, Mama Salma Kikwete ameapishwa rasmi leo Bungeni Dodoma.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Komentar untuk "KIKWETE ASHANGILIWA KWA ZAIDI YA DAKIKA KUMI ALIPOINGIA BUNGENI LEO"

Back To Top