VIDEO:NAWAONYA WATEKAJI MIMI KUTEKWA HAITOWEZAKANA -GODBLESS LEMA






Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amewaonya watu aliodai kuwa wamemuweka kwenye orodha ya wabunge kumi na moja wanaotakiwa kutekwa.

Akizungumza leo na waandishi wa habari mjini Dodoma, Lema amedai kuwa yeye haogopi vitisho vya kutekwa na kwamba wanaopanga kumteka wanapaswa kufahamu kuwa hawatafanikiwa na kwamba hakuna atakayeweza kusababisha kifo chake isipokuwa Mungu pekee.

“Ninawaonya watekaji, kwamba ninamjua Mungu ninaemwamini, kwamba hawataliona kaburi langu wala mauti yangu kwa sababu Mungu ninayemuamini najua nguvu zake na najua uwezo wake,” alisema Lema.

“Kwahiyo mimi kutekwa haitawezekana, kuuawa na mtu haitawezekana kwa sababu namtumaini Mungu kwa nguvu zangu zote,” aliongeza Mbunge huyo.
 
Tazama video hapa chini

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Komentar untuk " VIDEO:NAWAONYA WATEKAJI MIMI KUTEKWA HAITOWEZAKANA -GODBLESS LEMA "

Back To Top