Mbuge
wa Igunga Dk. Dalaly Peter Kafumu amefunguka na kusema kuwa wasaidizi
wa Rais wakiwemo wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mawaziri, na
wabunge wa upinzani na washauri wa karibu wa Rais wamekuwa wanafiki na
kushindwa kumshauri
Dalaly
ametoa kauli hiyo kwa madai ya kushindwa kumshauri vizuri Rais Magufuli
katika mambo ya msingi ambayo yanaweza kuleta maendeleo katika taifa
Dkt.
Kafumu amesema hayo bungeni wakati akichangia Bajeti ya Ofisi ya Waziri
Mkuu, mbunge huyo anasema viongozi hao wanashindwa kutumia vyema sifa
kuu tatu za Rais Magufuli ambazo ndizo zilikuwa zinahitajika kwa muda
mrefu.
"Tumepata
Rais ambaye sifa zake tatu zilikuwa zinahitajika sana, sifa ya kwanza
ana nia thabiti ya kuleta maendeleo kwa wanyonge, sifa ya pili anaamua
papo kwa papo hacheleweshi, sifa ya tatu anataka watu wafanye kazi, sifa
hizi sisi baadhi yetu tumezitumia vibaya tumeshindwa kuzitumia vyema
ili nchi yetu isonge mbele. Baadhi yetu wabunge wa upinzani na CCM,
baadhi yetu mawaziri siyo wote na baadhi yetu wasaidizi wa Rais
tumeshindwa kusema kweli, tumeshindwa kushauri kwa ukweli tumekuwa
wanafiki na hili jambo litatuua sana" alisema Kafumu
Kafumu
anadai wengi wao wamekuwa wakitengeneza ushauri nusu nusu kwa Rais
jambo ambalo linafanya zile sifa zake tatu kuu zitumike vibaya, kwa
kufanya maamuzi kwenye jambo ambalo huenda halijakamilika.
"Rais
anaamua pale pale unafikiri kitatokea nini? tunahitaji uchambue ushauri
wako, uupime, uutengeneze ushauri uende umekamilika, na Rais wetu huyu
anayefanya papo kwa papo akiamua nchi inasonga mbele, sasa hivi haya
yote tunayoyaona ni kwa sababu ya unafiki umezidi miongoni mwetu" alisema Kafumu
0 Komentar untuk "MBUNGE WA CCM DK. DALALI KAFUMU AWAPONDA WABUNGE WA CCM NA WASAIDIZI WA RAISI "